Tumeshinda mbele ya Al Kholood

Kikosi chetu kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Al Kholood inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Saudi Arabia.

Mlinzi wa kushoto Gadiel Michael alitupatia bao la kwanza dakika ya 27 baada ya kupokea pasi kutoka kwa mshambuliaji Habib Kyombo.

Kiungo mshambuliaji Augustine Okrah alitupatia bao la pili dakika ya 44 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Gadiel.

Kipindi cha pili tuliendelea kuliandama lango la Al Kholood lakini hatukuweza kuongeza jingine na matokeo kubaki kama ilivyokuwa cha kwanza.

Kocha Zoran Maki aliwatoa Henock Inonga,Pape Sakho, Augustine Okrah, Beno Kakolanya, Habib Kyombo na kuwaingiza Erasto Nyoni, Clatous Chama, Moses Phiri, Jimmyson Mwanuke na Ally Salim.

Mchezo wa leo ni wanne wa kirafiki tangu tulivyotua hapa Misri kwa ajili ya kambi ya maandalizi kuelekea msimu mpya wa ligi 2022/23.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER