Tumeshinda dhidi ya Malindi

Bao pekee lililofungwa na kiungo mkabaji Nassor Kapama limetosha kutupa ushindi dhidi ya Malindi katika mchezo wa kirafiki uliopigwa Uwanja wa Amaan Visiwani Zanzibar.

Kapama alifunga bao hilo kwa kichwa dakika ya 13 akimalizia mpira wa kona uliopigwa na winga Peter Banda.

Banda alishindwa kuendelea na mchezo na kufanyiwa mabadiliko dakika ya 23 nafasi yake ikachukuliwa na Jimmyson Mwanuke kufuatia kupata maumivu ya bega.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi na kuliandama lango la Malindi lakini hata hivyo safu yao ya ulinzi ilikuwa na utulivu mkubwa.

Kocha Juma Mgunda aliwatoa Kapama, Nelson Okwa, Dejan Georgijevic na Augustine Okrah na Jonas Mkude na kuwaingiza Sadio Kanoute, Kibu Denis, John Bocco, Moses Phiri na Victor Akpan.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER