Tumeruhusiwa kujaza uwanja dhidi ya Orlando, viingilio vyatajwa

Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limeruhusu mashabiki wote 60,000 kujitokeza katika mchezo wetu wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Orlando Pirates utakaofanyika Aprili 17, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

CAF imekuwa na utaratibu wa kuruhusu idadi chache ya mashabiki kwa sababu ya tahadhari juu ya ugonjwa wa Covid-19.

Hii ni mara ya kwanza baada ya kupita muda mrefu kuruhusiwa kujaza uwanja tangu lilipoingia janga la ugonjwa huo.

Viingilio vimetangazwa kama ifuatavyo:

VIP A Sh 30,000
VIP B Sh 20,000
VIP C Sh 10,000
Mzunguko Sh 3,000

Tiketi zimeanza kuuzwa leo kupitia mitandao ya simu na lengo letu ni kuhakikisha tunaujaza uwanja ili Orlando wavute pumzi ya moto.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER