Tumerejea NBCPL

Baada ya kupita mwezi mzima leo tumerejea kwenye Ligi Kuu ya NBC na tunaikaribisha Kagera Sugar katika mchezo ambao utapigwa Uwanja wa Uhuru saa 10 jioni.

Mchezo wetu wa mwisho wa ligi tulicheza Novemba 9 katika Uwanja wa Uhuru dhidi ya Namungo FC.

Katika kipindi hicho tulikuwa na majukumu na mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo leo ndio tumerejea kwenye Ligi Kuu ya NBC kuikaribisha Kagera leo.

Benchikha asema timu ipo tayari……..

Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha amesema kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo huku akikiri utakuwa mchezo mgumu.

Benchikha amesema haifahamu vizuri Kagera lakini ameifuatilia na anategemea upinzani mkubwa lakini tumejipanga kupata alama zote tatu.

“Utakuwa mchezo mgumu, Kagera ni timu nzuri lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda ingawa haitakuwa kazi rahisi,” amesema Benchikha.

Ally Salim atoa neno……

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji mlinda mlango, Ally Salim amesema kwa upande wao wapo tayari kuhakisha wanapambana ili kupata pointi tatu kutoka kwa Kagera.

“Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho, tunajua itakuwa mechi ngumu, Kagera ni timu bora lakini tumejipanga kushinda,” amesema Ally.

Ni mechi ya kwanza ya NBC ya Benchikha….

Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha ataiongoza timu katika mchezo wa leo ukiwa ni wa kwanza kwakwe wa Ligi Kuu ya NBC.

Benchikha raia wa Algeria ameiongoza timu katika mechi mbili dhidi ya Jwaneng Galaxy na Wydad Casablanca ambazo zote ni za Ligi ya Mabingwa Afrika.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER