Tumepoteza…

Mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Kagera Sugar uliofanyika Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera umemalizika kwa kupoteza kwa bao moja.

Tulianza mchezo kwa kasi na kuliandama lango la Kagera huku tukimiliki sehemu kubwa na kutengeneza nafasi lakini wachezaji wetu walikosa umakini.

Endapo nyota wetu Mzamiru Yassin, Shomari Kapombe na Bernard Morrison wangekuwa watulivu katika nafasi tulizopata tungeenda mapumziko tukiwa mbele kwa mabao matatu.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi tena ambapo dakika ya 45 shuti kali lililopigwa na Morrison lilipaa juu kidogo ya lango la Kagera.

Dakika ya 70 Hamis Kiiza aliwapatia wenyeji bao hilo la ushindi baada ya shambulizi la kushtukiza kufuatia wachezaji wetu kupanda kwenda kushambulia.

Kocha Pablo Franco aliwatoa Morrison, Mzamiru, Rally Bwalya, Mohamed Hussein na Joash Onyango kuwaingiza Medie Kagere, John Bocco na Yusuf Mhilu, Erasto Nyoni na Hassan Dilunga.

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

  1. Kupoteza mchezo tunapoteza pamoja na tunashinda pamoja pia.
    Wachezaji walipambana kwa kadri walivyoona inafaa kwa lengo moja la kuhakikisha tunapata matokeo chanya japo haikuwa hivyo.

    Niwapongeze makocha, madaktari na wachezaji waliocheza na hata waliokuwa benchi pia uongozi wa Simba S.c kwa jitihada wanazozionyesha ili kutufurahisha mashabiki wao. Ni kweli tunapata matokeo yasiyoridhisha ila sioni kama sababu ya kuturudisha nyuma kwani hutokea kwenye futbol, japo sio jambo la kulizoea. Kwenye mapambano ya ubingwa nina imani bado tuna uwezo hivyo tushikamane.

    Mwisho sio kwa umuhimu, nilitamani kuona mwandishi akiandika tofauti kidogo badala ya kuwataja majina wachezaji na kuonyesha as if walipenda kutozitumia nafasi walizozipata
    kwani sio wote
    watafikiri sawa na wewe.Bila shaka walipambana kuhakikisha tunaoata matokeo lakini bahati haikuwa yao hivyo kuyataja majina na kuamini bila wao kukosa basi tungekuwa na magoli kadhaa; idadi sawa na idadi ya wachezaji. Ninaona ni kitu kinachoweza kuwaumiza hivyo ninashauri tu kutafuta namna ambayo haitakuwa na viashiria vya kuonyesha uzembe ama vinginevyo. Sikosoi kwani sina taaluma kama ya mwandishi, lakini nimejaribu tu kuliona hilo na hivyo kuliwasilisha.

    #nguvu moja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER