Tumepoteza ugenini mbele ya Raja

Mchezo wetu wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca uliopigwa katika Uwanja wa Mfalme Mohamed wa tano umemalizika kwa kupoteza kwa mabao 3-1.

Hamza Khabba aliwapatia Raja bao la kwanza dakika ya 43 baada ya kupokea pasi ya mpira wa kichwa iliyopigwa na Yusri Bouzok.

Jean Baleke alitupatia bao la kusawazisha dakika ya 48 kwa mpira wa ‘kuchop’ baada ya kupokea pasi ya Mzamiru Yassin kufuatia mlinda mlango wa Raja kutoka.

Khaba aliwapatia Raja bao la pili kwa mkwaju wa penati dakika ya 68 kufuatia mlinzi wa kati Joash Onyango kumchezea madhambi ndani ya 18.

Mohamed Boulacsout aliwapatia Raja bao la tatu dakika ya 86 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Mohamed Benguit muda mfupi baada ya kuingia kutokea benchi.

X1: Zniti, Mukadem, Hadhoudi, Badaoui, Bentayd (Labib 73′), Sabbar (Benguit 84′), Zrida, Hafidi (Mahakasi 60′), Habti (Boulacsout 73′), Bouzok, Khabba (Benjdida 84′)

Walioonyeshwa kadi: Bentayd 36′

X1: Manula, Kapombe (Israel 90+1), Gadiel, Joash, Henock, Erasto, Chama, Mzamiru, Baleke, Saido (Bocco 90+1), Kibu (Sakho 75′)

Walioonyeshwa kadi: Chama 36′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER