Tumepoteza mechi ya Derby dhidi ya Yanga

Mchezo wetu wa Ligi kuu ya NBC dhidi ya watani wa jadi Yanga umemalizika kwa kupoteza kwa mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Aziz Ki aliipatia Yanga bao la kwanza dakika ya 18 kwa mkwaju wa penati baada ya yeye mwenyewe kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Baada ya bao hilo tuliongeza kasi ya kutaka kusawazisha huku tukitengeneza nafasi kadhaa za kufunga lakini tulipoteza umakini.

Joseph Guede aliwapatia Yanga bao la pili dakika ya 39 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wetu.

Freddy Michael Kouablan alitupatia bao la kufuatia machozi dakika ya 74 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Clatous Chama.

X1: Diarra, Yao, Lomalisa (Kibabage 12′), Bacca, Job, Aucho, Nzengeli (Mkude 85′) , Mudathir (Okra 85′), Guede, Aziz Ki, Mzize

Walioonyeshwa kadi: Job, Mudathir 27′ Aucho, Guede 90+4

X1: Lakred, Israel, Zimbwe Jr, Che Malone Henock (Kazi 15′), Babacar (Mzamiru 75′), Kibu (Jobe 75′), Ngoma (Miqussone 57′), Kanoute, Saido (Freddy 57′), Chama

Walioonyeshwa kadi: Chama 56′ Babacar 65′ Mzamiru 90+6

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER