Tumepoteza Mchezo wa pili dhidi ya Turan PFK

Mechi ya pili ya kirafiki dhidi Turan PFK iliyochezwa katika Uwanja wa Soğuksu Spor Kompleksi umemalizika kwa kupoteza bao moja.

Turan walipata bao hilo kwa kichwa mapema dakika ya nne kupitia kwa Rodarik Miller baada ya kuunganisha mpira wa kona.

Baada ya bao hilo tuliendelea kushambuliana kwa zamu huku tukifika zaidi langoni kwao ingawa hatukuweza kutumia nafasi tulizopata.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi na kufanya jitihada za kutafuta bao la kusawazisha dakika za mapema ili kuturudisha mchezoni lakini haikuwezekana.

Dakika ya 60 kiungo mshambuliaji, Willy Essomba Onana alipoteza nafasi ya kutupia bao la kusawazisha baada ya kubaki na mlinda mlango Tamal akashindwa kutumbukiza mpira wavuni.

Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ alifanya mabadiliko ya kuwatoa Sadio Kanoute, Clatous Chama, Onana na kuwaingiza Fabrice Ngoma, John Bocco na Jean Baleke.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER