Tumepoteza mchezo wa mshindi wa tatu

Mchezo wetu wa kutafuta mshindi wa tatu wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Bayelsa Queens kutoka Nigeria umemalizika kwa kupoteza kwa bao moja.

Mchezo ulianza kwa kasi tukishambuliana kwa zamu huku mpira ukichezwa zaidi katikati ya uwanja.

Kipindi cha pili Bayelsa walirudi kwa kasi huku tukionekana kukosa muunganiko na kufanya makosa ambayo yaliifanya safu yetu ya ulinzi kuwa mashakani muda mwingi.

Julieth Sunday aliwapatia Bayelsa bao hilo pekee dakika ya 71 baada ya mlinzi wa kati Esther Mayala kuchelewa kuondoa mpira wa krosi uliopigwa kutoka upande wa kulia.

Kocha Charles Lukula alifanya mabadiliko ya kuwaingiza Topister Situma, Olaiya Barakat, na Pambani Kuzoya na kuwatoa Asha Djafar, Esther Mayala na Philomena Abakahmshin.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER