Tumepoteza mchezo dhidi ya Horoya

Mchezo wetu wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya uliopigwa Uwanja wa Jenerali Lansana Conte nchini Guinea umemelizika kwa kupoteza kwa bao moja.

Wenyeji Horoya walipata bao hilo dakika ya 18 kupitia kwa Pape Ndiaye kwa kichwa akimalizia mpira wa kona uliopigwa na Mohamed Wonkoye.

Baada ya bao hili hatukupaniki tulicheza kwa kutulia pasi ndefu na mipira ya juu huku kasi yetu ikiwa ya kawaida kipindi cha kwanza.

Mlinda mlango Aishi Manula alicheza mkwaju wa penati dakika ya 72 uliopigwa na Ndiaye baada ya mlinzi Joash Onyango kuunawa mpira ndani ya 18.

Dakika ya 79 nahodha John Bocco almanusura atupatie bao la kusawazisha kufuatia mpira wake kutoka nje kidogo ya lango la Horoya baada ya kupokea pasi ya Kibu Denis.

Mchezo wetu unaofuata utakuwa Februari 18 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco.

X1: Camara, Coullibaly, Samassekou, Samake, Diaw, Kante (Naby 77), Camara, Wonkoye (Sebe 62′) Soumah (Coumbassa 86′), Ndiaye (Amamou 77′) Camara ( Ismael Camara 77′).

Walioonyeshwa kadi: Coullibaly 65′ Fode Camara 90.

X1: Manula, Kapombe Zimbwe Jr, Onyango, Henock, Kanoute, Sakho (Bocco 45′), Sawadogo (Phiri 61′), Baleke (Kibu 61), Mzamiru, Chama.

Walioonyeshwa kadi: Zimbwe Jr 60′, Kanoute 64′ Onyango 70′ Bocco 73′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER