Tumepoteza mbele ya wenyeji ASFAR

Timu yetu ya Simba Queens imepoteza kwa bao moja dhidi ya wenyeji ASFAR FC ya Morocco katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mchezo ulianza kwa kasi ya kadiri huku timu zikishambuliana kwa zamu huku mpira ukichezwa zaidi katikati ya uwanja

Ibtissam Jraidi aliwapatia wenyeji bao la kwanza dakika 66 kwa kichwa akimalizia mpira mrefu wa krosi uliopigwa na mlinzi wa kushoto Ghizlane Chebbak.

Baada ya bao hilo tulitengeza nafasi na kufanya mashambulizi kadhaa lakini tulikosa umakini wa kumalizia.

Kocha Charles Lukula alifanya mabadiliko ya kuwaingiza Koku Kipanga na Olaiya Barakat kuchukua nafasi za Vivian Corazone na Pambani Kuzoya.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER