Tumepoteza mbele ya mtani

Mchezo wetu wa Ngao ya Jamii kuashiria kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu ya NBC dhidi ya watani wetu uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa umeisha kwa kupoteza kwa mabao 2-1.

Pape Sakho alitupatia bao la kwanza dakika ya 16 akiwa ndani ya 18 baada ya kumalizia mpira wa krosi ulipigwa na Clatous Chama.

Baada ya bao hilo Yanga waliamka na kufanya mashambulizi ambayo hata hivyo yaliishia kwa walinzi wetu huku mlinda mlango Beno Kakolanya akiwa salama.

Fiston Mayele aliisawazishia Yanga bao hilo dakika ya 49 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Stephen Aziz Ki.

Mayele aliwapatia Yanga bao la pili la ushindi dakika ya 80 kwa shuti kali la mguu wa kushoto nje ya 18 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wetu.

Kocha Zoran aliwaingiza Nelson Okwa, Augustine Okrah Mzamiru Yassin, Dejan Georgijevic, John Bocco na kuwatoa Kibu Denis, Clatous Chama, Sadio Kanoute, Habib Kyombo, Jonas Mkude.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER