Tumepoteza mbele ya Al Hilal

Mchezo wetu wa mwisho wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Al Hilal umemalizika kwa kupoteza kwa bao moja mtanange uliopigwa Uwanja wa Al Hilal nchini Sudan.

Mchezo huo ulianza kwa kasi ya kadiri huku timu zote zikisomana na mpira ukichezwa zaidi katikati ya uwanja.

Mlinzi wa kushoto Gadiel Michael alishindwa kuendelea na mchezo na kutolewa dakika ya 17 baada ya kuumia nafasi yake ikachukuliwa na Nelson Okwa.

John Mano aliwapatia Al Hilal bao hilo pekee kwa kichwa dakika ya 61 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Ahmed.

Baada ya bao hilo tulifanya mashambulizi kadhaa langoni mwa Hilal ambayo mengi hayakuwa na nguvu na kuishia kwa walinzi wa wapinzani.

Kutokana na idadi kubwa ya wachezaji wetu kuwa majeruhi Kocha Zoran Maki alifanya mabadiliko mawili ya kuwatoa Gadiel ambaye aliumia na Augustine Okrah na kuwaingiza Okwa na Moses Phiri.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER