Tumepoteza dhidi ya Tanzania Prisons Jamhuri

Mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tanzania Prisons umemalizika kwa kupoteza kwa mabao 2-1 mtanange uliopigwa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.

Mchezo huo ulikuwa mkali huku tukishambuliana kwa zamu lakini itabidi tujilaumu wenyewe kutokana na kupoteza nafasi nyingi tulizotengeneza.

Mshambuliaji Samson Mbangula aliwapatia Prisons bao la kwanza dakika ya 45 baada ya kukokota mpira kutoka katikati ya uwanja na kupiga shuti liliomshinda mlinda mlango Aishi Manula.

Mbangula aliongeza bao la pili dakika ya 61 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wetu wa kati na kumzidi ujanja Manula.

Fabrice Ngoma alitupatia bao la kufutia machozi dakika ya 89 kwa shuti kali akiwa ndani ya 18 baada ya kumalizia mpira wa kona uliopigwa na Edwin Balua.

Kocha Abdelhak Benchikha alifanya mabadiliko ya kuwatoa Kibu Denis, Mzamiru Yassin, Freddy Michael, Henock Inonga na Babacar Sarr na kuwaingiza Pa Omary Jobe, Said Ntibazonkiza, Ladaki Chasambi, Hussein Kazi na Edwin Balua

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER