Tumepoteza Derby ya Mzizima

Mchezo wetu wa Ligi kuu ya NBC dhidi ya Azam FC ‘Mzizima Derby’ uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa umemalizika kwa kupoteza bao moja.

Mchezo ulianza kwa kasi ya kadiri timu zikishambuliana kwa zamu ambapo dakika ya 13 alimanusura Habib Kyombo atupatie bao baada ya kuushindwa kumalizia pasi ya Augustine Okrah.

Prince Dube aliwapatia Azam bao hilo pekee dakika ya 34 akimalizia pasi ya James Akaminko na kupiga shuti lililomshinda mlinda mlango Aishi Manula.

Dakika 15 za kwanza za kipindi cha pili Azam walikaa nyuma zaidi kujilinda wakituacha tucheze huku wakifanya mashambulizi machache ya kushtukiza.

Kocha Juma Mgunda aliwatoa Kyombo, Okrah, Jonas Mkude na Nassor Kapama kuwaingiza John Bocco, Peter Banda, Kibu Denis na Pape Sakho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER