Tumepata Ushindi mnono mbele ya Geita Kirumba

Kikosi chetu kimefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Nahodha John Bocco alitupatia bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 11 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Shomari Kapombe.

Clatous Chama alitupatia bao la pili dakika ya 41 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Mzamiru Yassin kabla ya kumzidi ujanja mlinzi wa kati wa Geita, Kelvin Yondani.

Dakika ya kwanza kipindi cha pili Pape Sakho alitupatia bao la tatu kwa shuti kali nje kidogo ya 18 kufuatia kupokea pasi ya Chama.

Sakho alipigilia bao nne dakika ya nne ya 75 kwa shuti kali nje 18 kufuatia mlinda mlango wa Geita kuzuia shambulizi la Chama.

Kibu Denis alikamilisha karamu ya mabao kwa kutupia la tano dakika ya 89 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Chama.

Kocha Juma Mgunda aliwatoa Sadio Kanoute, Bocco, Sakho na Henkck Inonga na kuwaingiza Victor Akpan, Kibu, Erasto Nyoni na Mohamed Ouattara.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER