Tumepata ushindi dhidi ya Telecom

Mchezo wetu wa kirafiki dhidi ya Telecom FC uliopigwa Uwanja wa Mercure umemaliza kwa kupata ushindi wa mabao 2-1.

Mpira ulianza kwa kasi huku timu zikishambuliana kwa zamu huku kila moja ikionekana kutafuta bao la mapema lakini safu za ushambuliaji zilipoteza umakini.

Dakika ya 18 wenyeji Telecom walipata bao la kuongoza lililofungwa kwa kichwa na Ashour Shika, aliyeunganisha mpira wa krosi.

Baada ya bao hilo tuliendelea kufanya mashambulizi lakini Telecom walikuwa makini huku wakicheza zaidi kwa kujilinda.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi na kuongeza presha kwenye lango la Telecom ambapo dakika dakika ya 62 Valentino Mashaka alitupatia bao la kusawazisha baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Valentine Nouma.

Kocha Fadlu Davids alifanya mabadiliko ya kuwatoa Freddy Michael, Augustine Okajepha, Ladaki Chasambi na.kuwaingiza Awesu Awesu, Willy Onana na Valentino Mashaka.

Dakika ya 77 kocha Fadlu alifanya mabadiliko ya kumtoa mlinzi Valentine Nouma na kumuingiza tena Chasambi.

Chasambi alitupatia bao la pili dakika ya 88 kwa kufunga kwa tiktak baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Kelvin Kijili.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER