Tumepata ushindi dhidi ya Pan African

Kikosi chetu kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Pan African katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Mo Simba Arena.

Mchezo huu wa kirafiki wa kimazoezi umechezwa katika vipindi vitatu yaani dakika 30 kila kipindi.

Said Ntibazonkiza alitupatia bao la kwanza dakika ya 35 kwa mkwaju wa penati baada ya yeye mwenyewe kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Moses Phiri alitupatia bao la pili dakika ya 65 baada ya kupokea pasi safi kutoka kiungo mshambuliaji, Willy Essomba Onana.

Kibu Denis alitupatia bao la tatu dakika ya 70 kufuatia Onana kuukosa mpira akiwa ndani ya 18 kabla ya kumkuta.

Onana alikamilisha karamu ya mabao kwa kufunga la nne dakika ya 87 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Phiri.

Kikosi kilichopangwa:

Ayoub Lakred (Ally 42′) (Abel 72), Shomari Kapombe (Duchu 60′), Mohamed Hussein (Israel 45′), Kennedy Juma (Kazi 55′), Che Malone (Kapama 60′), Mzamiru Yassin (Moses 55′), Fabrice Ngoma (Abdallah 55′), Clatous Chama (Onana 45), Jean Baleke (Chilunda 45′) (Jimmyson 72′), Saidi Ntibazonkiza (Kanoute 45′), Luis Miquissone (Kibu 30′) (Mohamed 72).

Walioonyeshwa kadi: Kazi 59′ Kanoute 87′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER