Tumepata ushindi dhidi ya Ngome

Kikosi chetu kimefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 6-0 dhidi ya Ngome katika mchezo wa kirafiki uliopigwa Uwanja wa Mo Simba Arena.

Moses Phiri alikosa mkwaju wa penati dakika ya tisa baada ya Luis Miquissone kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Shomari Kapombe alitupatia bao la kwanza dakika ya 31 kwa shuti kali ndani ya 18 baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Ngome.

Aubin Kramo alitupatia bao la pili dakika ya 41 baada ya mlinzi wa Ngome kujichanganya na mlinda mlango wake katika jitihada za kuokoa.

Jean Baleke alitupatia bao la tatu dakika ya 45 baada ya kupokea pasi safi kutoka Willy Onana.

Onana alitupatia bao la nne dakika ya 66 kwa mkwaju wa penati baada ya yeye mwenyewe kuchezewa madhambi ndani ya 18.

Baleke alikupatia bao la tano dakika ya 87 baada ya kumzidi ujanja mlinzi wa Kati Ngome.

Shaban Chilunda alikamilisha karamu ya mabao kwa kufunga la sita dakika ya 89 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Mohamed Mussa.

X1: Lakred (Ally 45′), Kapombe, Zimbwe Jr (Israel 59′), Kazi (Mwanuke 84′), Che Malone, Ngoma (Abdallah 71′) Kramo (Baleke 42′), Kanoute (Duchu 77′) Phiri (Kapama 60′) Miquissone (Chilunda 66′), Onana (Mohamed 75:)

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER