Tumepata ushindi dhidi ya Kipanga

Tumepata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kipanga FC katika mchezo wa kirafiki uliopigwa katika Uwanja wetu wa Mo Simba Arena.

Mchezo ulianza kwa kasi huku tukiliandama lango la Kipanga na kutengeneza nafasi nyingi ambazo hatukizitumia vizuri.

Moses Phiri alitupatia bao la kwanza dakika ya 21 baada ya kupokea pasi safi ya ‘fundi’ Clatous Chama.

Mlinzi wa kati, Henock Inonga ameoneshwa kadi ya njano dakika ya 30 baada ya Kumchezea madhambi mshambuliaji wa Kipanga, Kombo Ramadhani.

Winga, Luis Miquissone alitupatia bao la pili dakika ya 41 baada ya mpira uliopigwa na Sadio Kanoute kumgonga mlinzi wa Kipanga kabla ya kumkuta mfungaji.

Aubin Kramo alitupatia bao la tatu kwa mpira wa adhabu uliotinga wavuni moja kwa moja dakika ya 74 baada ya yeye mwenyewe kufanyiwa madhambi.

X1: Ally (Lakred 45′), Kapombe (Duchu 65), Zimbwe Jr (Israel 52′), Che Malone, Henock (Mwanuke 86′) Ngoma, Chama (Abdallah 65′), Kanoute (Kapama 85′), Phiri (Baleke 52′), Miquissone (Kramo 52′), Onana (Kazi 69′)

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER