Kikosi chetu kimeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa kirafiki wa kimazoezi uliopigwa katika Uwanja wa KMC Complex.
Mchezo huo ulikuwa mkali huku timu zote zikishambuliana kwa zamu lakini safu za ulinzi zilikuwa imara kuondoa mashambulizi.
Kiungo mshambuliaji Jean Charles Ahoua alitupatia bao la kwanza kwa mkwaju wa penati dakika ya 24 baada ya mlinzi mmoja wa JKT kuunawa mpira uliopigwa na Leonel Ateba.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kama ilivyokuwa cha kwanza huku timu zikitengeneza nafasi ambazo ufanisi wa kuzitumia ulikuwa mdogo.
Saleh Karabaka alitupatia bao la pili dakika ya mwisho ya nyongeza baada ya kumalizia kazi nzuri iliyofanywa na Valentino Mashaka.
Hiki hapa kikosi kilichoanza:
28. Manula, 12. Kapombe, 29. Nouma, 14. Hamza 20. Che Malone 21. Kagoma 38. Kibu 17. Deborah 13. Ateba 10. Ahoua 7. Mutale
Kipindi cha pili kocha Fadlu alifanya mabadiliko ya kukibadili kikosi kilichoanza isipokuwa mlinda mlango Aishi Manula.
Kocha Fadlu amewaingiza Kelvin Kijili, Saleh Karabaka, Karaboue Chamou, Hussein Kazi, Augustine Okajepha, Ladaki Chasambi, Fabrice Ngoma, Valentino Mashaka, Omary Omary na Awesu Awesu na David Kameta.