Tumepata sare ugenini

Mchezo wetu wa pili wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy uliopigwa Uwanja wa Obeid Ituni Chilume nchini Botswana umemalizika kwa sare ya bila kufungana.

Tulianza mchezo kwa kasi ambapo katika dakika tano za kwanza tulitengeneza nafasi tatu ambazo kama tungezitumia vizuri tungekuwa na uongozi mzuri wa mabao.

Tuliendelea kumiliki mchezo huku tukitengeneza nafasi ambazo hatukizitumia vizuri huku wenyeji Galaxy wakifanya mashambulizi machache ya kushtukiza.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi huku tuliendelea kutengeneza nafasi lakini kama kawaida tulishindwa kuzitumia.

Hata hivyo itabidi tujilaumu wenyewe kwa sare hii kufuatia mshambuliaji Jean Baleke akipoteza nafasi ya wazi dakika ya 84 ambayo ingeweza kutupa alama tatu.

X1: Lakred, Kapombe, Zimbwe Jr (Israel 90+2), Henock, Che Malone, Ngoma, Kibu (Miqussone 77′), Kanoute (Mzamiru 61′), Baleke, Ntibazonkiza (Phiri 77′), Onana (Chama 61′)

Walioonyeshwa kadi: Kanoute 45+2′ Henock 46′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER