Tumepata sare na KMC

Mchezo wetu wa tatu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi KMC uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa umemalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Moses Phiri alitupatia bao la kwanza mapema dakika ya pili baada ya kuwapiga chenga walinzi wa KMC nakupiga shuti kali lililomshinda mlinda mlango Nourdine Balora.

Baada ya bao hilo kasi ya mchezo iliongezeka huku tukishambuliana kwa zamu lakini tukitumia zaidi mipira mirefu kupitia pembeni kwa mawinga.

Mlinda mlango Balora alionyesha umahiri mkubwa baada ya kuokoa mipira miwili ya adhabu iliyopigwa na Augustine Okrah.

Matheo Anthony aliisawazishia KMC bao hilo dakika ya 47 baada ya mlinzi Israel Patrick kurudisha mpira mfupi kwa mlinda mlango Aishi Manula uliomkuta mfungaji.

Dakika 10 baadaye George Makang’a aliwapatia KMC bao la pili kwa shuti kali ndani ya 18 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wetu.

Habib Kyombo alitupatia bao la kusawazisha dakika ya 89 baada ya kumalizia mpira wa kichwa uliopigwa na John Bocco na kuguswa na Mohamed Ouattara ndani ya 18.

Kocha Seleman Matola aliwatoa Okrah, Nassor Kapama, Sadio Kanoute, Pape Sakho na kuwaingiza John Bocco, Mzamiru Yassin, Kibu Denis na Habib Kyombo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER