Tumepata sare na KMC

Mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya KMC uliopigwa Uwanja wa Azam Complex umemalizika kwa sare ya kufungana mabao 2-2.

Mchezo huo ulikuwa wa kasi na kuivutia tulimiliki sehemu kubwa lakini hata hivyo hatukuweza kuzitumia.

Waziri Junior aliwapatia KMC bao la kwanza dakika ya 30 baada ya kumzidi ujanja beki Che Malone.

Said Ntibazonkiza alitupatia bao la kusawazisha dakika ya 58 kwa mkwaju wa penati baada ya Abdulkarim Mohamed kuunawa mpira ndani ya 18.

Jean Baleke alitupatia bao la pili dakika ya 59 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Shomari Kapombe.

Waziri Junior aliwafungia KMC bao la pili dakika ya 88 baada ya shuti kali lililopigwa na Tepsi Evance kutemwa na kipa Ayoub Lakred.

Kocha Mkuu Abdelhak Benchikha alifanya mabadiliko yakuwatoa John Bocco, Willy Onana, Saido Ntibazonkiza, Sadio Kanoute na kuwaingiza Jean Baleke, Abdallah Khamis, Jimmyson Mwanuke na Luis Miqussone.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER