Tumepata pointi tatu za Singida Big Stars

Kikosi chetu kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Singida Big Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Jean Baleke alitupatia bao la kwanza dakika ya nane baada ya kumaliza mpira wa adhabu uliopigwa na Chama.

Saido Ntibazonkiza alitupatia bao la pili kwa kichwa dakika ya 20 baada ya kumalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Chama.

Bruno Gomes aliwapatia Singida bao la kwanza dakika ya 34 kwa mpira wa adhabu uliotinga wavuni moja kwa moja na kumshinda mlinda mlango, Aishi Manula.

Pape Sakho alitupatia bao la tatu dakika ya 63 kwa tik tak baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Shomari Kapombe.

X1: Manula, Kapombe, Zimbwe Jr, Onyango, Henock (Kennedy 87′), Kanoute (Sawadogo 83′), Sakho, Mzamiru, Baleke (Bocco 84′) Ntibazonkiza, Chama

Walioonyeshwa kadi: Kanoute 36′

X1: Haule, Gyan, Kibabage, Carno, Wawa, Kagoma, Andambwile (Ndemla 32′), Nashon, Kazadi, Bruno, Kagere (Fegu)

Walioonyeshwa kadi: Kagoma 41′ Carno 68′.Wawa, Bruno

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER