Mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Geita Gold umemalizika kwa kufanikiwa kupata ushindi wa bao moja katika mtanange uliopigwa Uwanja wa CCM Kirumba.
Mpira ulianza kwa kasi huku tukishambulia kwa kasi huku tukitengeneza nafasi kadhaa lakini tulishindwa kuzitumia
Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi huku Geita wakirudi nyuma muda na kufanya mashambulizi machache ya kushtukiza.
Babacar Sarr alitupatia bao la ushindi dakika ya 81 baada ya kumalizia mpira wa kichwa uliopigwa na Kibu Denis.
X1: Constantine, Mwaita, Mligo, Muha, Mahamud, Onditi, Julius, Ulaya (Dunia 69′), Kapera, Chikola, Edmund
Walioonyeshwa kadi: Ulaya 21′ Onditi 60′
X1: Manula, Kapombe, Zimbwe Jr, Kennedy, Che Malone, Ngoma, Kibu (Israel 90+3) Mzamiru (Ntibazonkiza 45′), Jobe (Fred 66′), Kanoute (Sarr 66′), Chama (Miqussone 66′)
Walioonyeshwa kadi: Kennedy 73′