Tumepata pointi tatu muhimu kwa Mkapa

 

Kikosi chetu kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Saido Ntibazonkiza alitupatia bao la kwanza dakika ya 10 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa fundi Clatous Chama aliyepokea mpira wa Bocco.

Bao hilo lilidumu kwa dakika mbili tu kwani City walisawazisha dakika ya 12 kupitia kwa Richardson Ng’ondya aliyepokea pasi ya Salim Kihimbwa.

Ntibazonkiza alitupatia bao la pili kwa mkwaju wa penati dakika ya 48 baada ya mlinzi Mohamed Hussein kuchezewa madhambi ndani ya 18 na Ng’ondya.

Pape Sakho alitupatia bao la tatu dakika ya 55 kwa shuti kali nje ya 18 baada ya kupokea pasi ya Ntibazonkiza aliyempora mpira Ng’ondya.

City ililalazimika kucheza wakiwa pungufu kwa dakika 25 za mwisho baada ya mlinzi wa kati Samson Madeleke kuonyeshwa kadi ya pili ya njano kwa kumchezea madhambi Sakho dakika ya 65.

City walipata bao la pili dakika ya 78 kupitia kwa mlinzi Juma Shemvuni kwa mpira mrefu katikati ya uwanja baada ya mlinda mlango Aishi Manula kusogea mbele na kuliacha lango.

X1: Manula, Kapombe, Zimbwe Jr, Onyango, Ouattara, Kanoute, Kyombo (Erasto Nyoni 91′), Mzamiru, Bocco (Kibu Denis 33′) Ntibazonkiza, Chama (Pape Sakho 33′)

Wachezaji wa Akiba ambao hawakutumika: Beno Kakolanya, Gadiel Michael, Nassor Kapama, Jimmyson Mwanuke.

Walionyeshwa kadi: Kanoute 43′ Mzamiru 57′ Onyango 67′ Manula 79′ Sakho 94′

X1: Kanyonga, Kunambi, Mwankemwa, Madeleke, Shemvuni, Ndunguli (Abdulrazak Mohamed 73′) Ng’ondya (Eliud Ambokile 63′) Hassan Nassor, Tariq, Awadh Juma (Sixtus Sabilo 62), Kihimbwa (Jamal Dullaz 84′)

Wachezaji wa Akiba ambao hawakutumika: Haroun Mandanda, Eradius Salvatory, Baliko Anyimke, Gaspar Mwaipasi, Baraka Mwalubunju.

Walionyeshwa kadi: Hassan Nassor 46′ Madeleke 52′ 66′ (nyekundu) Tariq Seif 67′ Kenneth Kunambi 71′.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER