Tumepata Pointi tatu Meja Jenerali Isamuhyo

Kikosi chetu kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao moja katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya JKT Tanzania uliopigwa Uwanja wa Meja Jenerali Michael Isamuhyo.

Mchezo ulianza kwa kasi huku tukishambuliana kwa zamu na kutengeneza nafasi lakini tukashindwa kuzitumia.

Clatous Chama alitupatia bao la kwanza dakika ya 34 kwa shuti kali la nje ya 18 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Saido Ntibazonkiza.

Kipindi cha pili tuliongeza kasi ya mashambulizi lakini hata hivyo tulishindwa kuyatumia.

Mzunguko wa kwanza wa Ligi umemalizika tukiwa nafasi ya pili tukiwa na alama 36 baada ya kucheza mechi 15.

X1: Jacob, Kigi, Bryson, Sadock, Katanga, Hassan, Magulu (Songo 89′), Ndemla (Matiko 74′), Sabilo (Kapalata 56′), Matheo, Kichuya (Kada 56′)

Walioonyeshwa kadi: Kigi 23′ Hassan Maulid 56′

X1: Lakred, Kapombe, Zimbwe Jr, Kennedy,  Che Malone, Babacar, Ntibazonkiza (Israel 89′) Kanoute (Mzamiru 69′), Kibu (Fred 57′), Ngoma (Jobe 89′), Chama (Miqussone 89′)

Walioonyeshwa kadi: Freddy 65.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER