Tumepata pointi tatu kwa KVZ

 

Kikosi chetu kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao moja dhidi ya KVZ katika mchezo wa pili wa Michuano ya Kombe la Mapinduzi uliopigwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Mchezo ulianza kwa kasi ya kawaida ukichezwa zaidi katikati ya uwanja huku tukishambuliana kwa zamu lakini tulimiliki sehemu kubwa ya mchezo.

Mshambuaji Michael Joseph alitupatia bao hilo pekee kwa kichwa dakika ya 40 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Augustine Okrah.

Kipindi cha pili hakukuwa na mabadiliko makubwa ambapo tuliendelea kulishambulia lango la KVZ lakini bado tulikosa utulivu.

Kocha Juma Mgunda alifanya mabadiliko ya mchezo mmoja ambapo alimtoa Nelson Okwa na kumuingiza Joseph Mbaga.

Katika mchezo huo mfungaji wa bao pekee Joseph Michael ameibuka mchezaji bora na kukabidhiwa kitita cha Sh. 500,000 kutoka kwa wadhamini.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER