Tumepata pointi tatu Ali Hassan Mwinyi

Kikosi chetu kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora.

Pa Omar Jobe alitupatia bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 19 baada ya kumalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Clatous Chama.

Sadio Kanoute alitupatia bao la pili kwa kichwa dakika ya 36 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Shomari Kapombe.

Che Malone alitupatia bao la tatu dakika ya 59 akiwa ndani ya 18 baada ya kumalizia pasi ya Chama.

Fred Michael alitupatia bao la nne dakika ya 88 baada ya kumzidi ujanja mlinzi wa Tabora na kupiga shuti lililomshinda mlinda mlango John Noble.

X1: Noble, Maulid, Mbatty, Lulihoshi, Bikoko, Milandui, Mbombo, Najim, Okutu, Lambele, Nakibinge

Walioonyeshwa kadi: Nakibinge 56′ Lolihoshi 65′

X1: Lakred, Kapombe, Zimbwe Jr, Kennedy, Che Malone, Babacar (Duchu 85′) Kibu (Balua 85′), Kanoute (Mzamiru 69′), Jobe (Fred 69′), Ntibazonkiza (Miqussone 75′), Chama

Walioonyeshwa kadi: Kanoute 41′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER