Tumepata mwaliko maalumu kutoka Al Hilal

Kikosi chetu kimepokea mwaliko maalumu kutoka kwa Klabu ya Al Hilal ya Sudan kushiriki michuano maalum ambayo itaanza kufanyika wiki ijayo.

Tukiwa nchini Sudan tutacheza mechi mbili dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana, Agosti 28 na wenyeji Al Hilal Agosti 31, mwaka huu.

Mechi hizi za kimataifa tutazitumia kama sehemu ya maandalizi wakati ligi ikiwa imesimama kupisha mechi za kufuzu Fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN).

Wachezaji tisa walioitwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayojiandaa na mchezo dhidi ya Uganda hawatakuwa sehemu ya safari.

Timu inatarajia kuondoka nchini Alhamisi alfajiri kuelekea nchini Sudan tayari kuwahi mechi ya kwanza itakayopigwa Agosti 28, dhidi ya Asante Kotoko.

Mtendaji Mkuu wa Klabu, Barbara Gonzalez ameishukuru Al Hilal kwa mwaliko huo ambao unaendeleza ushirikiano na mshikamano ambapo wenyeji wamegharamia kila kitu.

“Kipekee niwashukuru Al Hilal kwa mwaliko huu, licha ya kuongeza ushirikiano baina yetu lakini pia itakipa mazoezi mazuri kikosi chetu kipindi hiki ligi ikiwa imesimama kwahiyo tunakuwa tumepata faida mara mbili,” amesema Barbara.

Baada ya kukamilika kwa Mashindano kikosi kitarejea nchini na Septemba 3 kitacheza mechi nyingine ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Mabingwa wa Djibouti, AS Arta Solar 7 mbayo iko kambini jijini Dar es Salaam ikiwa na nyota kama Alexander Song na Solomon Kalou.

Al Hilal imeendeleza ushirikiano baina yetu ambapo mwaka 2021 tuliwaalika katika Michuano ya Simba Super Cup ambayo tuliandaa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER