Tumepata alama moja Songea

Mchezo wetu wa mwisho wa Ligi Kuu ya NBC uliofanyika Uwanja wa Majimaji mjini Songea dhidi ya Mbeya Kwanza umemalizika kwa sare ya bila kufungana.

Mchezo ulianza kwa kasi timu zikishambuliana kwa zamu lakini ulikuwa unachezwa zaidi katikati ya uwanja kwa ufundi mkubwa.

Mlinda mlango wetu Beno Kakolanya aliokoa mipira kadhaa iliyokuwa ya hatari wakati Kibu Denis akipoteza nafasi za kufunga ambazo zingetufanya kwenda mapumziko tukiwa mbele.

Kipindi cha pili tuliongeza kasi ya kutafuta bao la ushindi lakini tulikosa umakini katika eneo la mwisho na mashambulizi yakaishia kwa mlinda mlango wa Mbeya Kwanza.

Kocha Seleman Matola aliwatoa Kassim Omary na Yusuf Mhilu na kuwaingiza Henock Inonga na John Bocco.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER