Tumepangwa na Nyasa Big Bullets ya Malawi

Droo ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika imekamilika na tumepangwa na Mabingwa wa Malawi Nyasa Big Bullets ambapo tutaanzia ugenini.

Mchezo huo ni wa hatua ya awali ya michuano hiyo ambapo kama tukifanikiwa kushinda tukutana na mshindi kati ya Red Arrows za Zambia na Primero De Agosto ya Angola.

Big Bullets ilianzishwa mwaka 1967 na ni miongoni mwa timu zenye mashabiki wengi nchini Malawi na imetwaa ubingwa wa mara 16.

Nyota wetu Peter Banda ametokea timu mwaka 2021 hii ambayo amecheza kwa mwaka mmoja kabla ya kutolewa kwa mkopo katika timu ya Sheriff Tiraspol kutoka Moldova.

Mchezo wa kwanza utapigwa katika kati ya Septemba 9-11 nchini Malawi na marudiano yatakuwa Septemba 16-18.

Big Bullets nao wanatumia jezi nyekundu wakiwa nyumbani na nyeupe ugenini kama tulivyo si.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER