Droo ya hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika imekakilmilika na tumepangwa na miamba ya soka Al Ahly kutoka Misri.
Mchezo wa mkondo wa kwanza utapigwa kati ya Machi 29 na 30 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa huku ule wa marudiano ukipigwa kati ya Aprili 5 na 6 jijini Cairo.
Msimu huu tumekutana na Al Ahly katika michuano mipya ya African Football League (AFL) ambapo miamba hiyo pia ilitutoa kwa faida ya bao la ugenini.
Mshindi wa jumla kati yetu na Al Ahly atakutana na mshindi kati ya TP Mazembe na Petro De Luanda ya Angola.