Tumepangwa Kundi C Mapinduzi Cup

 

Ratiba ya michuano ya Kombe la Mapinduzi ambayo hufanyika Visiwani Zanzibar imetoka na tumepangwa Kundi C ambalo litakuwa na timu tatu.

Kila mwaka michuano hiyo huanzia mwanzoni mwa mwaka na kukamilika siku moja baada ya sherehe za Mapinduzi ambazo hufanyika Januari 12.

Msimu huu michuano ya Mapinduzi itashirikisha timu 12 huku tano zikitoka Tanzania Bara, Sita kutoka Visiwani na moja kutoka nchini Burundi.

Sisi ndio mabingwa watetezi na tumepangwa pamoja na timu za Mlandege pamoja na KVZ zote kutoka Visiwani Zanzibar.

Mchezo wetu wa kwanza utakuwa Januari 3 dhidi ya Mlandege na Januari 5 tutamaliza na KVZ.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER