Tumeondoka na Pointi zote mbele ya Azam kwa Mkapa

Kikosi chetu kimefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Feisal Salum alikosa mkwaju wa penati dakika ya 34 kufuatia winga Gibril Syllah kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Sadio Kanoute alitupatia bao la kwanza dakika ya 64 kwa shuti kali akiwa ndani ya 18 kufuatia mpira wa krosi uliopigwa na Mzamiru Yassin kuzuiwa na mlinzi Fuentes.

Fabrice Ngoma alitupatia bao la pili kwa kichwa dakika ya 77 baada ya kumalizia mpira wa adhabu uliopigwa na nahodha Zimbwe Jr.

David Kameta ‘Duchu’ alitupatia bao la tatu bao la tatu ya 89 kwa shuti kali ndani ya 18 baada ya mpira uliopigwa na Freddy Michael kugonga mwamba kabla ya kumkuta mfungaji.

Ushindi huu unatufanya kufikisha pointi 56 baada ya kucheza mechi 25 tukiendelea kusalia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi.

X1: Lakred, Israel, Zimbwe Jr, Kennedy Che Malone, Ngoma, Balua (Duchu 74′), Mzamiru, Freddy, Kanoute (Hamis 90+2′), Chasambi (Onana 82′)

Walioonyeshwa kadi: Kanoute 55′ Ngoma 65′ Duchu

X1: Mustafa, Chilambo, Msindo, Bangala, Funtes, Zayd (Lyanga 78′), Syllah, Akaminko (Mtasigwa 78′), Kipre Jr, Feisal, Nado (Sopu 71′)

Walioonyeshwa kadi: Chilambo 70′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER