Ushindi wa bao moja tuliopata dhidi ya JKT Tanzania katika Uwanja wa Meja Jenerali Michael Isamuhyo siku ya Alhamisi umekamilisha mzunguko wa kwanza wa Ligi ya NBC.
Mchezo huo ulikuwa wa 15 na kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi tukifikisha pointi 36 tukiwa nafasi ya pili kwenye msimamo.
Katika michezo hiyo tumeshinda 11 tumetoka sare mitatu na kupoteza mmoja.
Said Ntibazonkiza ndiye kinara wa ufungaji kwenye kikosi chetu akiwa amefunga mabao matano akifuatiwa na Clatous Chama mwenye manne.
Hii hapa Orodha ya wafungaji
Mabao Assist
Ntibazonkiza 5 3
Chama 4 3
Kanoute 2 0
Bocco 1 0
Kibu 1 0
Ngoma 1 0
Jobe 1 0
Babacar 1 0
Fred 1 0
Kapombe 0 4
Zimbwe Jr 0 3