Mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania (TWPL) umemalizika huku kikosi cha Simba Queens kikiwa kileleni mwa msimamo.
Ligi ya Wanawake ambayo inashirikisha timu 10 imesimama kupisha maandalizi ya timu ya Taifa ya Twiga Stars kujiandaa na michuano ya kufuzu Olimpiki dhidi ya Afrika Kusini ‘Banyana Banyana’.
Simba Queens imemaliza mzunguko huo ikiwa na alama 25 baada ya kucheza mechi tisa ikishinda nane na kutoka sare moja.
Katika michezo hiyo Queens imefunga mabao 33 huku ikiruhusu kufungwa mabao matano.
Matokeo ya mechi zote tisa za Simba Queens
Simba Queens 5 – 0 Ceassia Queens
Simba Queens 5 – 2 baobab queens
Simba Queens 3 – 1 Yanga Princess
Simba Queens 3 – 0 JKT Queens
Amani Queens 2 – 3 Simba Queens
Bunda Queens 0 – 0 Simba Queens
Simba Queens 7 – 0 Alliance Girls
Fountain Gate Princess 0 – 4 Simba Queens
Geita Queens 0-3 Simba Queens