Tumemaliza msimu wa 2023/24 kwa ushindi

Rasmi Leo tumekamilisha msimu wa Ligi Kuu ya NBC 2023/24 kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mchezo ulianza kwa kasi huku tukishambuliana kwa zamu lakini umakini ulikosekana huku zikitengenezwa nafasi nyingi kadhaa za kufunga lakini hazikutumiwa.

Kipindi cha pili tuliongeza kasi zaidi na kutengeneza nafasi nyingi huku JKT wakicheza nyuma zaidi na kufanya mashambulizi machache ya kushtukiza.

Saido Ntibazonkiza alitupatia bao la kwanza kwa mkwaju wa penati dakika ya 88 baada ya mlinzi mmoja wa JKT kuunawa mpira ndani ya 18.

Willy Onana alitupatia bao la pili dakika ya mwisho ya nyongeza baada ya kupokea pasi safi kutoka Fabrice Ngoma na kumpiga chenga mlinda mlango wa JKT.

Matokeo haya yanatufanya kufikisha pointi 69 tukiwa nafasi ya tatu na msimu ujao tutashiriki Kombe la Shirikisho barani Afrika.

X1: Lakred, Kapombe, Zimbwe Jr, Kennedy, Che Malone, Ngoma, Chasambi, Mzamiru (Onana 75′), Ntibazonkiza, Miqussone (Karabaka 69, Balua (Chama 45′)

Walionyeshwa kasi: Che Malone 25″

X1: Yakoub, Kilemile, Bryson, Katanga, Haidari, Ndemla, Sabilo, Macheza, Lyanga (Matheo 45′), Kapalata, Kada

Walioonyeshwa kadi: Bryson 36′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER