Kikosi chetu kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Power Dynamos kutoka Zambia katika mchezo wa kilele cha Simba Day uliofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Will Onana alitupatia bao la kwanza mapema dakika ya nne baada ya kupiga shuti kali nje kidogo ya 18 baada kupokea pasi ya Saido Ntibazonkiza.
Baada ya bao hilo tuliendelea kulishambulia la Power huku nao wakija kwetu mara chache kwa kushtukiza.
Kipindi cha pili tuliongeza kasi hasa baada ya mabadiliko aliyofanya kocha mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ ingawa hatukizitumia vizuri.
Fabrice Ngoma alitupatia bao la pili dakika ya 75 kwa kichwa akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na Said Ntibazonkiza kufuatia kona fupi iliyopigwa na Luis Miquissone.
X1: Ally (1), Kapombe (12), Zimbwe Jr (15), Che Malone (20), Inonga (Kazi 60-) (29), Kanoute (8) (Khamis 80′), Onana (Baleke 58′) Mzamiru (Ngoma 58) (19), Kibu (38) (Kramo 80′) Ntibazonkiza (Bocco 80′) (10), Chama (17) (Miquissone 58:)
Walioonyeshwa kadi: Baleke 61′ Ngoma 81′
X1: Mwanza (30), Chiboni (4), Bakodile (5), Makwaza Jr (Muwowo 63′) (6), Mutale (Tembo 50′) (7), Mulomba (Chideu 45′)(8), Katebe (14), Mulombw (17), Bong (18), Phiri (Soko 50′) (22), Bongeli (39) (Kaunda 72′).
Walioonyeshwa kadi: Tembo 50′ Katebe 63′ Chiboni 77′