Tumekabidhiwa ‘Mzigo wa mama’ baada ya kutua Dar

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa ametukabidhi pesa taslimu Sh. 5,000,000 ‘Mzigo wa mama’ ikiwa ni ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan kununua kila bao linalofungwa na wawakilishi wa nchi kwenye michuano ya CAF.

Rais Samia anatoa Sh. 5,000,000 kwa kila bao linalofungwa na wawakilishi wa nchi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa na Shirikisho ili kuongeza morali.

Msigwa amemkabidhi kitita hicho Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu, Ahmed Ally ambaye muda huo huo alimpatia nahodha John Bocco ili akagawane na wachezaji wenzake.

Makabidhiano hayo yamefanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) muda mfupi baada ya kikosi kuwasili kutoka nchini Morocco.

Katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa katika Uwanja wa Mfalme Mohamed wa Tano juzi Machi 31 tulifanikiwa kufunga bao moja huku wenyeji Raja wakifunga matatu na ndio maana tukapewa kitita hicho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER