Tumekabidhiwa milioni tano kutoka kwa Rais Samia

Baada ya ushindi wa bao moja tuliopata dhidi ya Wydad Casablanca katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika tumekabidhiwa Shilingi 5,000,000 ikiwa ni sehemu ya motisha kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan.

Rais Samia amekuwa akitoa kiasi hicho cha pesa kwa kila bao tunalofunga kwenye michuano hii ili kuongeza morali kwa timu za Tanzania kufanya vizuri.

Pesa hiyo amekabidhiwa nahodha, John Bocco na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Tulia Akson ambaye alikuwa Mgeni Rasmi wa mchezo wetu.

Katika mchezo uliopita wa nyumbani dhidi ya Horoya kutoka Guinea tulikabidhiwa Sh. 35,000,000 baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 7-0.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER