Tumekaa Kileleni mwa NBCPL

Ushindi wa mabao 3-1 tuliopata dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya umetufanya kupaa hadiĀ  kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.

Ushindi huu umetufanya kufikisha pointi 12 baada ya kushinda mechi zote nne za mwanzo za ligi Kuu.

Edwin Baluwa aliwapatia Tanzania Prisons bao la kwanza kwa mpira wa adhabu uliotinga moja kwa moja wavuni baada ya Che Fondoh Malone kufanya madhambi nje kidogo ya 18.

Clatous Chama alitupatia bao la kusawazisha dakika ya 34 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Shomari Kapombe.

Nahodha John Bocco alitupatia bao la pili dakika ya nyongeza kipindi cha kwanza baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Mzamiru Yassin.

Said Ntibazonkiza alitupatia bao la tatu kwa mkwaju wa penati dakika ya 86 baada ya mshambuliaji Moses Phiri kufanyiwa madhambi na mlinda mlango, Yona Amosi ndani ya 18.

X1: Ally, Kapombe, Zimbwe Jr, Kennedy, Che Malone, Ngoma, Chama (Kanoute 88′), Mzamiru, Bocco (Phiri 83′), Ntibazonkiza (Chilunda 88′), Kibu (Onana 88′),

Walioonyeshwa kadi: Mzamiru 90+3′

X1: Yona, Kimenya, Samson, Elfadhili, Chilo, Balua, Meshack (Mbangula 45′), Sabiyanka, Masenga (Zabona 83′), Batshi (Messi 83′) Jeremia

Walioonyeshwa kadi: Kimenya 84′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER