Tumejipanga kurejesha hali ya kujiamini kwa Namungo

Baada ya kupitia kipindi kigumu cha kutopata matokeo tunayoyatarajia tumejipanga kuhakikisha tunaibuka na ushindi dhidi ya Namungo FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC ili kurudisha hali ya kujiamini.

Kocha msaidizi Seleman Matola, amesema wachezaji wetu wanapoteza nafasi nyingi uwanjani kutokana na kucheza kwa presha kitu ambacho kinaendelea kufanyiwa kazi mazoezini.

Matola amesema tunakosa muda wa kufanyia marekebisho makosa yanatokea kutokana na mechi kufuatana lakini kuelekea mchezo wa kesho kutakuwa na mabadiliko makubwa ya kiuchezaji.

“Tunapitia kipindi kigumu, wachezaji wanacheza kwa presha ndiyo maana tunapoteza nafasi nyingi lakini tunaendelea kulifanyia kazi na kuelekea mechi ya kesho kutakuwa na mabadiliko makubwa,” amesema Matola.

Matola amesema wachezaji wapo katika hali nzuri na morali ipo juu tayari kuhakikisha tunapata ushindi kwa kuonyesha soka safi kama kawaida.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER