Tumejipanga kivita nchini Zambia

Kocha Mkuu Pablo Franco, amekiri mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Red Arrows utakaopigwa Jumapili nchini Zambia utakuwa mgumu lakini tumejipanga kuwakabili.

Pablo amesema anajua Red Arrows wataingia uwanjani kutaka kupindua matokeo lakini tuna mtaji mzuri wa mabao hivyo tumejipanga kuhakikisha tunalinda ushindi wetu.

Raia huyo wa Hispania ameyasema hayo akiwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere pamoja na kikosi wakiwa tayari kuelekea Zambia kwa ajili ya mchezo huo.

“Tunajua mchezo utakuwa mgumu, Red Arrows watataka kushinda lakini tumejipanga kupambana nao, kikubwa tunahitaji kulinda ushindi wetu tuliopata mchezo uliopita.

“Wachezaji wote wako kwenye hali nzuri na morali ipo juu na tunafahamu kitu gani kinatakiwa kuelekea mchezo wa Jumapili ili kuwapa furaha mashabiki wetu,” amesema Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER