Tumeingiza mguu mmoja Nusu Fainali Shirikisho

Ushindi wa bao moja tuliopata katika uwanja wa nyumbani dhidi ya Orlando Pirates umetufanya kuingiza mguu mmoja katika Nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Tulianza mchezo kwa kasi kwa kuliandama lango la Orlando na kumiliki sehemu kubwa kwa kutengeneza nafasi lakini ufanisi wetu haukuwa mzuri.

Orlando walicheza kwa kujilinda zaidi wakijaza watu wengi katika eneo lao huku wakifanya mashambulizi machache ya kushtukiza.

Mlinzi wa kulia Shomari Kapombe alitupatia bao la kwanza kwa mkwaju wa penati dakika ya 68 baada ya Bernard Morrison kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Kocha Pablo Franco aliwatoa Peter Banda, Taddeo Lwanga, Morrison, Pape Sakho na Chris Mugalu kuwaingiza Kibu Denis, Rally Bwalya, Mzamiru Yassin, Yusuf Mhilu na Medie Kagere.

Kutokana na hatua hiyo, kwa sasa tutahitaji ushindi au sare ya aina yoyote katika mchezo wa marudiano utakaofanyika nchini Afrika Kusini ili tufuzu nusu fainali.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER