Tumeichapa KMC na kuupiga mwingi kwa Mkapa

Pamoja na ushindi mnono wa mabao 3-1 tuliopata dhidi ya KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa kikosi chetu kimecheza kandanda safi lililowavutia mashabiki waliohudhuria.

Tulianza mchezo kwa kasi kwa kuliandama lango la KMC lakini wote walikuwa nyuma kuzuia huku wakifanya mashambulizi ya haraka ya kushtukiza.

Hassan Kabunda aliwapatia KMC bao la kwanza dakika ya 40 baada ya shuti kali lililopigwa na Matheo Anthony kumgonga Pascal Wawa kabla ya kumkuta mfungaji.

Kibu Denis alitusawazishia bao hilo dakika ya 51 baada kumalizia kazi nzuri iliyofanywa na Pape Sakho aliyewapiga chenga walinzi wa KMC na kupiga krosi ya chini chini ndani ya 18.

Sakho alitupatia bao la pili dakika ya 62 baada kumalizia pasi ya Kibu kufuatia shambulizi alilolianzisha mwenyewe.

Mlinzi wa kati Henock Inonga alitupatia bao la tatu kwa kichwa dakika ya 65 baada ya kumalizia krosi iliyopigwa na Sakho.

Kocha Seleman Matola aliwatoa Sadio Kanoute, Kibu, Sakho, Erasto Nyoni na Rally Bwalya na kuwaingiza Peter Banda, Medie Kagere, Jimmyson Mwanuke, Taddeo Lwanga na Yusuf Mhilu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER