Tumeibuka na ushindi dhidi ya Kipanga

Kikosi chetu kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kipanga FC katika mchezo wa kirafiki uliopigwa Uwanja wa Amaan hapa Zanzibar.

Katika mchezo huo, Augustine Okrah alitupatia bao la kwanza dakika ya 36 kwa mpira wa adhabu uliotinga moja kwa moja wavuni aliopiga akiwa nje kidogo ya 18.

Okrah tena alitupatia bao la pili kwa mkwaju wa penati dakika ya 62 baada ya mlinzi wa kulia Israel Patrick kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Kibu Denis alitupatia bao la tatu dakika ya 64 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Israel kutoka upande wa kulia.

Kocha Juma Mgunda alifanya mabadiliko ya kuwatoa Okrah na Gadiel Michael na kuwaingiza Victor Akpan, Mohamed Hussein.

Winga Jimmyson Mwanuke alishindwa kuendelea na mchezo na kutolewa dakika 13 baada ya kupata majeraha na nafasi yake ikachukuliwa na Kennedy Juma.

Baada ya mchezo wa leo kikosi kinarejea jijini Dar es Salaam tayari kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Dodoma Jiji utakaopigwa Oktoba 2 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER