Mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Azam FC uliopigwa Uwanja wa New Amaan Complex Visiwani Zanzibar umemalizika kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Mchezo huo ulianza kwa kasi huku tukiliandama lango la Azam huku nao wakijibu mashambulizi mara kadhaa.
Leonel Ateba alitupatia bao la kwanza dakika ya 15 kwa shuti kali la mguu wa kushoto baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Jean Charles Ahoua.
Fabrice Ngoma alitupatia bao la pili dakika ya 47 kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na Ahoua kuunganishwa kwa kichwa na Kibu Denis na kuokolewa na mlinda mlango Mustafa Mohamed kabla ya kumkuta mfungaji.
Baada ya bao hilo tuliendelea kuliandama lango la Azam na kufanya mashambulizi kadhaa lakini milango ilikuwa migumu kufunguka.
Ushindi huu unatufanya kufikisha pointi tisa baada ya kucheza mechi tatu huku tukifunga mabao tisa tukiwa hatujaruhusu nyavu zetu kuguswa.
X1: Mohamed, Mwaikenda, Msindo, Fuentes, Yoro, Mtasingwa, Syllah (Sidibe 63′) Akaminko, Saadun (Blanco 85′), Feisal, Nado (Diakite 79′)
Walioonyeshwa kadi: Nado 14′
X1:Camara, Kapombe Zimbwe Jr Che Malone Hamza, Ngoma, Kibu (Kijili 72′), Fernandez (, Ateba (Mukwala 63′), Ahoua (Awesu 63′), Mutale (Balua 63′)
Walioonyeshwa kadi: