Mchezo wetu wa mwisho wa kirafiki dhidi ya Al-Adalah inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza nchini Saudi Arabia uliopigwa Uwanja wa New Suez Canal umemalizika kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Mchezo huo ulianza kwa kasi huku timu zikishambuliana kwa zamu ambapo mshambuliaji Steven Mukwala alitupatia bao mapema dakika ya tisa baada ya kumalizia pasi safi iliyopigwa na Fabrice Ngoma.
Joshua Mutale alitupatia bao la pili dakika ya 32 baada ya kupokea pasi kutoka Ngoma tena.
Kipindi cha pili Al- Adalah walirudi kwa kasi na walifanikiwa kupata penati baada ya kipa Ally Salim kufanya madhambi ndani ya 18.
Kocha Fadlu Davids alifanya mabadiliko ya kuwatoa Mukwala, Mzamiru Yassin, Edwin Balua, Shomari Kapombe na kuwaingiza Valentino Mashaka, Awesu Awesu, Augustine Okajepha na Kelvin Kijili.